• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania na China zapongeza ushirikiano kuhifadhi wanyamapori

    (GMT+08:00) 2018-02-07 10:36:29

    Maofisa na wadipolomasia kutoka Tanzania na China jana wamepongeza ushirikiano uliopo kati ya nchi hizo mbili kwenye uhifadhi wa wanyamapori.

    Maofisa hao pia wameahidi kuimarisha zaidi ushirikiano kati yao kwenye Mkutano wa Baraza la China na Tanzania kuhusu uhifadhi wa wanyamapori na maendeleo ya utalii uliofanyika mjini Dar es Salaam.

    Katibu mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii ya Tanzania Bw. Gaudence Milanzi amesema, Tanzania inaichukulia China kuwa mwenzi wake muhimu kwenye uhifadhi wa wanyamapori. Amesema mustakabali wa uhifadhi wa wanyamapori unategemea ushiriki wa wadau mbalimbali katika kupanga na kutekeleza hatua za kupambana na ujangili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako