• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Katibu mkuu wa UN alaani matumizi ya silaha za kikemikali nchini Syria, atoa wito umoja kwa baraza la usalama

  (GMT+08:00) 2018-02-07 17:57:32

  Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Antonio Guterres amelaani matumizi ya silaha za kikemikali nchini Syria na kutoa wito kwa baraza la Usalama kuhahikisha wahusika wanachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria.

  Kwa mujibu wa taarifa ya katibu mkuu huyo iliyotolewa na naibu msemaji wake bwana Farhan Haq, Guterres pia amelaani vikali matumizi yoyote ya silaha za aina hiyo ambayo kamwe hayawezi kuhalalishwa.

  Bw. Guterres amerudia wito wa kuungana pamoja kwa baraza la usalama kuhakikisha wahusika wote wa matumizi ya silaha za kikemikali wanatambuliwa na kufikishwa mbele ya sheria.

  Mwaka jana Russia ilitumia kura yake ya turufu mara tatu kupinga utaratibu wa kuendeleza uchunguzi wa pamoja uliokuwa unafanywa na Umoja wa Mataifa kwa kushirikiana na Shirika linalopiga marufuku silaha za kikemikali OPCW, na mwezi uliopita ikapendekeza mpango mpya wa kuchunguza, lakini wajumbe wa baraza walionekana kutilia shaka.

  Naibu Balozi wa kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa Bw. Wu Haitao, jana alisema China inaunga mkono jitihada za Russia za kusisitiza kuundwa kwa mpango mpya wa uchunguzi. China pia ina matumaini kuwa wajumbe wa baraza hilo wataendelea kushauriana ili kufikia muafaka mapema iwezekanavyo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako