• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Burundi akanusha ripoti kuhusu China zinazopotosha ukweli

    (GMT+08:00) 2018-02-08 14:29:35

    Rais Pierre Nkurunziza wa Burundi jana amekutana na waandishi wa habari wa China kwenye Ikulu ya nchi hiyo huko Bujumbura, na kutoa salamu za mwaka mpya kwa watu wa China.

    Kwenye mkutano huo, Rais Nkurunziza amesema, China siku zote inatoa misaada katika nyanja mbalimbali zikiwemo elimu, afya na ujenzi wa miundo mbinu nchini Burundi, na ushirikiano kati ya pande hizo mbili umetoa mfano mzuri wa kuigwa kwa nchi nyingine.

    Akizungumzia ripoti zilizotolewa hivi karibuni na vyombo vya habari vya nchi za magharibi kuwa China iliweka vifaa vya ujasusi kwenye jengo la Makao makuu ya Umoja wa Afrika mjini Addis Ababa, Ethiopia, rais Nkurunziza amesema, hiyo ni njia ya vyombo vya habari vya magharibi kuleta mvutano kati ya China na nchi za Afrika, na haina msingi wowote, na kusisitiza kuwa China ni mwenzi muhimu wa ushirikiano kwa nchi za Afrika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako