• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • WHO yaunda kikosi cha kukabiliana na matukio ya dharura ya huduma za afya duniani

    (GMT+08:00) 2018-02-08 19:31:28

    Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema, WHO itaunda kikosi cha kukabiliana na matukio ya dharura ya uhitaji wa huduma za afya duniani ambacho kinajumuisha maelfu ya wafanyakazi wa afya kutoka nchi 50.

    Bw. Tedros amewaambia waandishi wa habari kuwa, ujenzi wa uwezo wa kukabiliana na matukio ya dharura ya afya ni kazi muhimu zaidi katika zilizofanywa na shirika hilo tangu achaguliwe kuwa mkurugenzi mkuu. Hivyo shirika hilo limeanzisha baraza la afya la kujadiliana matukio ya dharura ya afya duniani kila baada ya wiki mbilin na kutoa ripoti kwa mkurugenzi mkuu wa shirika hilo kila siku kuhusu maendeleo ya matukio ya dharura ya afya duniani.

    Bw. Tedros amesema, nchi hizo 50 pia zitatoa msaada wa kifedha, vifaa, usafiri na ugavi. Amesisitiza kuwa, watu hao watabaki kwenye nchi zao, lakini kama matukio ya dharura ya kiafya yatatokea, basi WHO itafanya uratibu. .

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako