• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kiwango cha usalama wa jamii nchini China chaongoza duniani

  (GMT+08:00) 2018-02-09 16:20:59

  China imekubalika kuwa ni moja ya nchi salama zaidi kote duniani, lakini gharama zinazotumika na serikali ya China katika kulinda usalama wa jamii ni chini ya kiwango cha wastani cha kimataifa. Hivyo ni kwa namna gani China imeweza kudumisha usalama wa ndani? Carol Nasoro ana zaidi.

  Mwaka 2017, China ilikuwa moja ya nchi zenye kiwango cha chini cha uhalifu wa mauaji kote duniani, na idadi ya matukio mabaya ya kimabavu yaliyotokea mwaka huo ilipungua kwa zaidi ya nusu kuliko mwaka 2012, hali inayofanya asilimia 95.55 ya watu wa China kuridhika na hali ya usalama nchini. Profesa Wang Dawei wa chuo kikuu cha usalama wa umma cha China anaona kuwa, kwa vigezo vyovyote vile, kiwango cha usalama wa jamii nchini China kinachukua nafasi ya mbele duniani.

  "Hivi sasa kuna aina mbili za vigezo vya kupima usalama wa jamii, moja ni vigezo vya maoni ya umma ambavyo vinazingatia kiwango cha wanachi kujihisi salama na kuridhishwa na kazi za polisi, na pili ni vigezo vya takwimu ambavyo vinapima kiwango cha kutokea na kutatuliwa kwa matukio ya uhalifu. Kwa vigezo vyovyote vile vya usalama wa jamii, ikilinganishwa na kiwango cha kimataifa, China huchukua nafasi ya mbele duniani."

  Jambo linalofuatiliwa zaidi ni kwamba, hali nzuri ya usalama nchini China imepatikana kwa gharama ya chini. Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na mashirika ya Umoja wa Mataifa, idadi ya wastani ya polisi kwa kila watu laki moja katika nchi mbalimbali kote duniani ni mia tatu, lakini hapa China idadi hiyo ni 140 tu, ambayo iko chini zaidi kuliko kiwango cha wastani cha kimataifa.

  Profesa Wang Dawei anasema, kuhamasisha na kushirikisha umma kwenye usimamizi wa usalama ni mbinu maalumu inayotumiwa na China kuhakikisha usalama wake wa ndani. Anasema,

  "Mkakati wa kuhamasisha na kushirikisha umma kwenye usimamizi wa usalama ni mbinu bora inayotumika kwenye kazi ya kulinda usalama wa umma nchini China. Nadharia kuu kwenye mapinduzi ya nne ya mambo ya polisi ni kwamba, jamii ni chanzo cha uhalifu, na umma ni nguvu muhimu ya kuzuia uhalifu. Hivi sasa watu wengi wamejitolea kushiriki kwenye usimamizi wa usalama, na hali hii pia ni uvumbuzi tunaofanya kwenye usimamizi wa jumla wa kijamii unaoshirikisha zaidi umma. Tunatakiwa kuelewa kwa undani umuhimu na uzuri wa uvumbuzi huu, na kuendelea kuutekeleza."

  Mtindo huo mpya wa usimamizi wa jumla kwa usalama wa jamii wenye ufanisi wa juu na gharama za chini, si kama tu unatoa uzoefu kwa nchi nyingine duniani, na bali pia unatoa mchango muhimu katika kulinda amani na utulivu wa dunia.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako