• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Serikali ya Tanzania kununua pamba ya wakulima

  (GMT+08:00) 2018-02-09 19:09:09

  Serikali ya Tanzania imesema imeweka mkakati mahususi kuhakikisha pamba yote iliyozalishwa na wakulima wa zao hilo baada kuhamasishwa, itatununuliwa na wanunuzi wa ndani na nje ya nchi.

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alisema hayo baada ya bunge la nchi hiyo kutaka kujua jinsi serikali imejipanga katika kununua pamba yote ya wakulima ya kuhamasishwa na kuzalisha kwa wingi zao hilo.

  Bunge limesema wakulima wa zao hilo hivi sasa wanazalisha kutoka kilo 6,000 hadi kilo milioni 30.

  Bunge la Tanzania pia limeitaka serikali kuwasaidia wakulima kwa kuhakikisha kuwa dawa za kuua wadudu wanaoshambulia mimea ya zao hilo, inapatikana kwa urahisi na kwa wakati katika mikoayote inayokuza pamba.

  Hata hivyo Majaliwa amesema serikali inafanya mchakato wa kutafuta wanunuzi wa zao hilo nje ya nchi kupitia wizara ya kilimo inayoshughulikia jambo hilo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako