Sudan imemteua tena Bw. Salah Abdallah Gosh kuwa mkuu wa Idara ya ujasusi na usalama ya taifa NISS baada ya kuondoka kwa miaka tisa.
Bw. Gosh aliwahi kuwa mkuu wa NISS kuanzia mwaka 1999 hadi 2009, ambapo aliimarisha ushirikiano kati ya NISS na Shirika la ujasusi la Marekani CIA.
Baada ya kuondoka kwenye idara hiyo, Bw. Gosh alikuwa mshauri wa rais hadi mwanzoni mwa mwaka 2011.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |