• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Morocco na Umoja wa Mataifa zajadili kuhusu hatua za kuboresha hali ya usalama ya vikosi vya umoja huo barani Afrika

  (GMT+08:00) 2018-02-13 08:49:02

  Naibu waziri wa ulinzi wa Morocco Bw. Abdeltif Loudyi na mshauri wa kijeshi wa operesheni ya kulinda amani ya Umoja wa Mataifa Luteni Jenerali Calos Humberto Loitey wamejadili hatua za kuboresha hali ya usalama ya vikosi vya Umoja huo barani Afrika, na mchango wa Morocco katika operesheni za Umoja huo.

  Maofisa hao pia wamejadili kuhusu hatua za kuimarisha utekelezaji wa operesheni za kulinda amani kutokana na mazingira magumu yanayozikabili operesheni zinazofanywa hivi sasa.

  Bw. Loudyi amesisitiza juhudi muhimu na endelevu zilizofanywa na Morocco katika sekta ya kulinda amani, huku akisifia mipango iliyozinduliwa na katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres ikiwa sehemu ya mageuzi ya utaratibu wa Umoja wa Mtaifa kwa ulinzi wa amani na usalama.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako