• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa nchini DRC chakabiliwa na tuhuma mpya za uhalifu wa kingono

  (GMT+08:00) 2018-02-13 08:58:17

  Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Stephane Dujarric amesema, Kikosi cha Kulinda Amani cha Umoja huo nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC kimepokea malalamiko mapya manne ya utendaji mbaya, ikiwemo malalamiko matatu ya uhalifu wa kingono.

  Bw. Dujarric amesema, tuhuma hizo zinawahusisha askari wa kulinda amani kutoka nchini Afrika Kusini. Pia amesema, tuhuma tatu za uhalifu wa kingono zinawahusu waathirika ambao ni watu wazima, na zilitokea katika miji ya Beni na Goma katika mkoa wa Kivu Kaskazini. Malalamiko mengine yanahusu maumivu ya mwili aliyopata kijana wa miaka 17 baada ya kupigwa na askari wa kulinda amani katika mkoa wa Kasai Mashariki nchini DRC.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako