• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Sudan yaanzisha tena biashara ya mpaka wa nchi hiyo na Sudan Kusini

  (GMT+08:00) 2018-02-13 09:11:24

  Sudan imetangaza rasmi kuwa itaanza tena biashara ya mpaka na Sudan Kusini, ikiwa ni utekelezaji wa maelekezo yaliyotolewa na Rais Omar al-Bashir wa Sudan.

  Ujumbe wa serikali ya Sudan ulioongozwa na waziri wa biashara Bw. Hatim al-Sir umetembelea Jimbo la White Nile kwenye mpaka na Sudan Kusini kwa lengo la kutangaza kuanza tena kwa biashara ya mpakani kati ya nchi hizo mbili.

  Mwezi April mwaka 2015, Sudan iliamua kufunga biashara ya mpakani na Sudan Kusini, ambayo imeshuhudia vita ya wenyewe kwa wenyewe tangu mwaka 2013.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako