• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Abbas akataa Marekani kuwa mpatanishi kuhusu suala la Palestina na Israel

  (GMT+08:00) 2018-02-13 17:54:44

  Rais Mahmoud Abbas wa Palestina amesema, anakataa Marekani kuwa mpatanishi kuhusu suala la Palestina na Israel.

  Rais Abbas ambaye yuko ziarani nchini Russia amesema hayo wakati alipokutana na mwenzake wa Russia Vladimir Putin. Rais Abbas amesema, tangu Donald Trump aingie madarakani, hatua za Marekani ikiwemo kufunga ofisi ya Chama cha Ukombozi wa Palestina PLO nchini Marekani na kutambua Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel zimewashtua watu wa Palestina. Amesema Palestina inapinga kithabiti hatua hizo za Marekani na kutotambua hadhi ya mpatanishi wa Marekani katika suala hilo.

  Rais Abbas pia amesema, kutokana na mabadiliko ya msimamo wa Marekani kuhusu suala hilo, nchi hiyo itafanya juhudi kujadili suala la Mashariki ya Kati na la Palestina na Israel pamoja na Russia, huku akiitaka Russia izidi kutoa mchango wa kiujenzi kwenye sekta hizo. Pia ameongeza kuwa Palestina inakubali mpango wa kufanya mazungumzo ya moja kwa moja kati ya viongozi wa pande hizo mbili uliotolewa na rais Putin.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako