• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • ANC yamlazimisha rais Zuma kujiuzulu

  (GMT+08:00) 2018-02-14 09:03:35
  Chama tawala cha Afrika Kusini ANC kimethibitisha kuwa kitamwondoa madarakani rais Jacob Zuma wa nchi hiyo. Katibu mkuu wa chama cha ANC Bw. Ace Magashule amewaambia waandishi wa habari kuwa, uamuzi huo umefikiwa jana katika mkutano wa Kamati Kuu ya ANC uliofanyika Johannesburg. Amesema kwa wiki kadhaa sasa, chama hicho kimefanya mawasiliano na rais Zuma kumtaka aondoke madarakani. Rais Zuma anatakiwa kutoa jibu lake hii leo. Ameongeza kuwa, kimsingi rais Zuma amekubali kujiuluzu, lakini amependekeza apewe muda wa kati ya miezi mitatu hadi sita.
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako