• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kenya inalenga kutumia njia ya kidijitali katika kuendesha kampeini ya kuwavutia watalii wengi zaidi nchini humo

  (GMT+08:00) 2018-02-14 09:45:57

  Kwa muda mrefu Mamlaka ya utalii ya Kenya imekuwa ikitumia vyombo vya habari vya kigeni pamoja na kufanya maonesho kwenye kampeini zaka za kuwavutia watalii nchini humo. Hata hivyo hivi sasa huenda mambo yakabadilika baada ya wizara ya utalii ya Kenya kupendekeza njia ya kidijitali katika kuwavutia watalii.Akizungumza kwenye mkutano na wadau wa utalii mjini Nairobi, waziri wa utalii wa Kenya Bw Najib Balala amesema njia ya kutumia programu za kidijitali ndio hakikisho pekee la kuwavutia watalii nchini Kenya.Balala ameongeza kuwa wataanza kutumia programu hiyo ifikapo machi mwaka huu.

  "Biashara haitokani na maonesho ya kibiashara, biashara inafanikishwa na mtandao wako mwenyewe pamoja na mikakati ya kidijitali ya kujiuza. Mbona tujitengeneze programu ya kidijitali ambayo tunaweza kutumia kuweka picha ya mnyama na inaweza kutupa maelezo yote kuhusu huyo mnyama.Tunatakiwa kufikia kiditali. Uzuri ni kuwa Kenya hususan Nairobi ina maendeleo makubwa sana ya kidijitali".

  Takwimu kutoka kwa Mamlaka ya utalii ya Kenya zinaonesha kuwa jumla ya watalii milioni 1.4 walizuru Kenya mwaka jana, ikiwa ni ongezeko la asimilia 10 ikilinganishwa na mwaka 2016.Serikali ya Kenya inalenga kuongeza idadi hiyo hadi milioni 3 kila mwaka ili mapato yaongezeke hadi shilingi bilioni 200 kila mwaka. Ili kufikiwa serikali za kaunti nazo zimetakiwa kuweka vivutio vya kitalii katika maeneo yao ili kufanikisha ndoto hiyo.Samuel Ole Tunai ni gavana wa kaunti ya Narok na ameahidi kulinda hifadhi ya wanyama ya Maasai Mara ikiwa ni sehemu ya juhudi za kufanikisha ndoto ya serikali.

  "Hili suala la kila mtu anataka kuweka kambi ndogo mahali ambapo kuna msitu ni lazima lisitishwe.Nafikiri baadhi yenu mmeshuhudia tukibomoa baadhi ya majengo ambayo yalikuwa yamewekwa kwenye misitu wa Maasai Marai

  Tamko hilo la Gavana wa Naroka linakuja wakati ambapo sekta ya utalii ya Kenya inaonekana kukua baada ya kushuhudia mawimbi makali yaliyochochewa na changamoto za kiusalama.Kila mwaka idadi ya watalii ambao wanawasili kwa meli imekuwa ikiongezeka na tayari waziri Balala ameahidi kujenga eneo la kifahari la kuwapokea wageni katika bandari ya Mombasa.

  "Kama hatutajitolea na kuwa na mipango mizuri kwa kushirikiana na wadau muhimu itakuwa vigumu sana. Hata hivyo nitashirikiana na wadau kuhakikisha kuwa hilo limefaulu. Hilo ndio linalonila kichwa kwa sasa".

  Kuongezeka kwa idadi ya watalii nchini Kenya kunadaiwa kuchangiwa na kuwepo kwa amani ikilinganishwa na miaka ya nyuma ambapo kulikuwa na uchaguzi na kisiasa.Idadi kubwa ya watalii wanatoka nchi za Poland, Italia, Ujerumani na Ufaransa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako