• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Sehemu kadhaa Kenya kukumbwa na mafuriko

  (GMT+08:00) 2018-02-15 16:31:07

  Wakuu wa utabiri wa hali ya hewa katika kanda ya afrika mashariki wameonya kwamba huenda kukatokea mafuriko nchini Kenya wakati wa msimu ujao wa mvua.

  Wwakizungumza mwishoni mwa mkutano wa siku mbili nchini Kenya aidha wakuu hao wamesema hata baada ya mvua bado kwa kipindi cha miezi 3 hivi watu kwenye upembe wa afrika wataendelea kukabiliwa na ukosefu wa chakula.

  Ronald Mutie anaripoti kutoka Nairobi.

  Mwezi wa Januari umekuwa na jua kali katika maeneo mengi nchini Kenya.

  Mvua zinatarajiwa baadaye mwezi huu hadi Mei.

  Lakini wanasayansi na watabiri wa hali ya hewa kutoka nchi 11 za upembe wa Afrika wameonya kwamba huenda maeneo ya pwani, Nairobi, Kaskazini Mashariki na Mashariki yakakumbwa na mafuriko.

  Wadau hao wametoa ripoti ya hali ya mvua za kati ya Machi na Mei mwaka huu, baada ya mkutano wao wa siku mbili mjini Mombasa.

  "Kuna uwezekano kwamba kutakuwa na mvua kubwa ambazo zitasababisha mafuriko hata katika maeneo ambako hupokea mvua zaka za kawaida . Pia kuna uwezekano wa kutokea ukame kwenye maeneo ambayo hupokea mvua za wastani "

  Kulingana na ripoti hiyo baadhi ya maeneo ya Pwani, Nairobi Kaskazini Mashariki na Mashariki yatakuwa na mafuriko.

  Aidha mkurungenzi wa idara ya utabiri wa hewa nchini Kenya Peter Ambenje anasema kuna uwezekano wa kuzuka kipindi cha lanina.

  "Utafiti unaonyesha tutapata hali za wastani. Maana yake ni kwamba ni hali ya katikati ya elnino na lanina "

  Lakini hii sio mara ya kwanza kwa wanasayansi kutoka ripoti sawa nah ii.

  Baada ya kutolewa kwa ripoti na onyo kama hilo mwaka jana, mvua na ukame uliofuatia uliwaacha zaidi ya watu milioni 20 wakikumbwa na njaa katika kanda ya upembe wa Afrika, hasa nchini Somalia na Sudan Kusini.

  Na sasa mkuu wa kitengo cha mabadiliko ya tabia nchi katika Mamlaka ya Serikali na Maendeleo IGAD Dkt. Guleid Artan anasema idadi hiyo imeongezeka.

  "Hadi kufikia leo kuna takriban watu milioni 27.5 wanaohitaji msaada wa chakula kwenye eneo hili la upembe wa Afrika"

  Bwana Peter Ambenje anasema hata wakati huu kukitarajiwa mvua bado makali ya ukame yataendelea kuathiri watu wengi Afrika mashariki hadi angalau mwezi Juni.

  "Katika maeneo ambako tayari kuna kiangazi ama kulikonyesha mvua kidogo bado watu watakabiliwa na hali ngumu. Kwa hivyo kati ya sasa na mwezi Mei hakutakuwa na mabadiliko makubwa hata baada ya mvua kunyesha"

  Washiriki wa mkutano huo wamezitaka serikali za Afrika Mashariki kutumia data kuhusu hali ya hewa ili kujiandaa vyema kukabili mabadiliko yoyote kama vile mafuriko au ukame.

  Baadaye wiki ijayo Kenya itatoa ripoti yake ya kina kuhusu hali ya hewa itatolwa wiki ijayo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako