• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Idara ya utabiri wa hali ya hewa imetahadharisha kuhusu mafuriko

    (GMT+08:00) 2018-02-15 16:29:35

    Wakulima na wafanyibiashara wa vyakula wametakiwa kujiandaaa na mvua kubwa itakayonyesha kuanzia mwezi ujao.

    Idara ya utabiri wa hali ya hewa imetahadharisha kuhusu visa vya mafuriko katika baadhi ya maeneo ya humu nchini kuanzia mwezi ujao.

    Mkurugenzi wa idara hiyo, Peter Ambenje amesema maeneo ya Pwani, Nairobi, Mashariki na Kaskazini Mashariki yataathiriwa zaidi na mafuriko kati ya mwezi Machi na Mei.

    Idara hiyo pia imesema nchi za Ethiopia, Sudan Kusini, Uganda, Rwanda na Tanzania pia zitakumbwa na wimbi la mafuriko.

    Ambenje alisema hayo kwenye kikao cha-48 cha kongamano kuhusu hali ya hewa katika eneo la upembe wa Afrika lililoandaliwa mjini Mombasa.

    Ambenje alisema kuna uwezekano mkubwa wa eneo hilo kupata mvua kubwa kuliko kiwango cha kawaida.

    Kongamano hilo pia lilihudhuriwa na wataalamu kutoka shirika la utabiri wa hali ya hewa duniani na taasisi ya kimataifa kuhusu hali ya hewa. Ambenje alizihakikishia nchi za Burundi, Djibouti, Eritrea, Ethiopia, Kenya, Rwanda, Somalia, Sudan Kusini, Sudan, Tanzania na Uganda kuwa shirika la utabiri wa hali ya hewa duniani litaziarifu kuhusu hali hiyo ya E-Nino.

    Ambenje ambaye ni mwakilishi wa shirika hilo nchini Kenya alisema utabiri huo utazisaidia nchi hizo kuweka mikakati ya kukabiliana na mikasa ambayo huenda ikatokea

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako