• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Kenya atoa salamu za mwaka mpya wa jadi wa China kwa wachina

    (GMT+08:00) 2018-02-15 16:40:31

    Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya ametoa salamu za mwaka mpya wa jadi wa China kwa wachina.

    Katika salamu zake Rais Kenyatta amesema katika zaidi ya miaka 600 iliyopita, ushirikiano kati ya Kenya na China umekuwa ukipata mafanikio mapya. Ameeleza imani kuwa uhusiano kati ya nchi hizo mbili utafungua ukurasa mpya katika mwaka huu mpya.

    Ameongeza kuwa China na Kenya zimeshirikiana kujenga miradi mingi muhimu ikiwemo wa reli ya Mombasa-Nairobi, ambayo inaboresha maisha ya wakenya.

    Wakati huohuo, katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres naye pia ametoa salamu za mwaka mpya wa jadi wa China kwa njia ya video. Ameishukuru China na wananchi wake kwa kuunga mkono kazi ya Umoja wa Mataifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako