• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini ajiuzulu kutokana na shinikizo

    (GMT+08:00) 2018-02-15 16:49:16

    Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini amejiuzulu wadhifa wake baada shinikizo kutoka kwa chama chake.

    Licha ya msimamo wa huko nyuma wa kuonyesha kukaidi, Rais Zuma alitangaza kujiuzulu saa moja kabla ya muda wa mwisho aliopewa na chama chake. Katika hotuba ya nusu saa ya kuaga taifa, Rais Zuma amesema ameamua kujiuzulu kwa kuwa hataruhusu chama cha ANC kigawanyike kutokana na jina lake.

    Amesema hakuna haja ya watu kupoteza maisha kutokana na jina lake, na kuwa licha ya kwamba hakubaliani na maamuzi ya viongozi wa chama, amekuwa ni mwanachama mwenye nidhamu wa ANC.

    Rais Zuma ameomba radhi kwa taifa kutokana na makosa yote yaliyofanyika wakati wa uongozi wake, lakini anaamini kuwa ametekeleza jukumu alilopewa na nchi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako