• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Jacob Zuma ajiuzulu

  (GMT+08:00) 2018-02-16 16:42:14

  Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma amejiuzulu wiki hii siku moja tu kabla ya bunge kujadili hoja ya kutokuwa na imani yake na pia baada ya shinikizo nyingi kutoka kwa chama chake cha ANC.

  Kapitia hotuba yake iliyopeperushwa kwa njia ya televisheni alisema anajiuzulu mara moja lakini akaongeza kuwa hakubaliani na uamuzi wa chama cha ANC.

  Chama cha ANC kilikuwa kimemuambia aondoke madarakani au akabiliwe na kura ya kutokuwa na imani naye bungeni.

  Zuma mwenye umri wa miaka 75 amekuwa akikabiliwa na shinikizo za kumtakja ampe nafasi mamamu wake Cyril Ramaphosa, ambaye ndiye sasa kiongozi mpya wa chama.

  Bw Zuma ambaye amekuwa madarakani tangu mwaka 2009, amekumbwa na shutuma nyingi za ufisadi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako