• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Palestina yatoa onyo kwa hatua za Israel za kukalia makazi ya Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan

  (GMT+08:00) 2018-02-16 16:45:01

  Ikulu ya Palestina imeonya kuwa hatua yoyote ya upande mmoja inayohusiana na Israel kukalia makazi ya Ukingowa Magharibi wa Mto Jordan haitabadilisha hali halisi kuwa makazi hayo ni haramu.

  Msemaji wa rais Bw. Nabil Abu Rudeineh ametoa taarifa akisema, hatua yoyote katika hilo itaongeza hali ya wasiwasi na ukosefu wa utulivu.

  Taarifa hiyo imetolewa kwa ajili ya kujibu ripoti za vyombo vya habari kwamba Israel inajadiliana na Marekani kuhusu uhalali wa kukalia makazi kwenye Ukingowa Magharibi wa Mto Jordan.

  Taarifa hiyo pia imesema, hatua kama hizo zitaharibu juhudi zote za kimataifa kuokoa mchakato wa amani.

  Kwingineko Rais Mahmoud Abbas wa Palestina amesema, anakataa Marekani kuwa mpatanishi kuhusu suala la Palestina na Israel.

  Rais Abbas ambaye yuko ziarani nchini Russia amesema hayo wakati alipokutana na mwenzake wa Russia Vladimir Putin. Rais Abbas amesema, tangu Donald Trump aingie madarakani, hatua za Marekani ikiwemo kufunga ofisi ya Chama cha Ukombozi wa Palestina PLO nchini Marekani na kutambua Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel zimewashtua watu wa Palestina.

  Amesema Palestina inapinga kithabiti hatua hizo za Marekani na kutotambua hadhi ya mpatanishi wa Marekani katika suala hilo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako