• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Wizara ya Sheria ya China yasema wafungwa 1,300 watachiwa kwa muda katika sikukuu ya Spring

  (GMT+08:00) 2018-02-16 16:45:18

  Wizara ya Sheria ya China imesema takriban wafungwa 1,300 kutoka magereza 300 ya hapa China wataachiwa kwa muda ili kujumuika na familia zao katika kipindi cha sikukuu ya Spring, ilioanza tarehe 16 Februari mwaka huu.

  Hiii ni sehemu ya mpango wa karibuni uliotolewa na wizara hiyo wa kurejesha mfumo wa kuachiliwa wafungwa wakati wa sikukuu uliositishwa katika miaka ya karibuni kutokana na hatari kubwa na sababu nyingine kadhaa.

  Katika taarifa ya karibuni, wizara inahitaji mamlaka za sheria za majimboni kuchagua wafungwa wenye tabia njema kama majaribio ya mpango na hatua kwa hatua kufanya mfumo huo uwe wa kawaida.

  Taarifa hiyo pia inahitaji uchunguzi wa kina wa tabia za wafungwa gerezani ili kuweza kuruhusiwa na kusimamiwa kwenye sikukuu kama hiyo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako