• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Shirika la kibinafsi la China latarajiwa kurusha satilaiti za "Mfumo wa Ladybug"

    (GMT+08:00) 2018-02-19 18:57:25

    Shirika la Jiutianweixing ambalo ni shirika binafsi la usafiri wa anga ya juu la China hivi karibuni limezindua rasmi mpango wake wa kurusha satilaiti saba za "Mfumo wa Ladybug" katika nusu ya pili ya mwaka huu. Mpango huo ni mkubwa zaidi ya usafiri wa anga ya juu uliofanywa na mashirika yasiyo ya kiserikali nchini China.

    Katika miaka ya hivi karibuni, shughuli za kibiashara za usafiri wa anga ya juu nchini China na katika mataifa mengine zinaendelea kwa kasi, mahitaji makubwa ya habari kutokana na utandawazi wa uchumi yanatiliwa maanani mashirika mbalimbali ya sayansi na teknolojia ya Marekani yakiwemo Google na SpaceX, huku mashirika ya Ulaya na China pia yametoa mpango husika.

    Mkurugenzi wa ofisi ya uendeshaji wa shughuli za elimu na hakimiliki ya taasisi ya utafiti wa mitambo ya mwanga ya hali ya juu ya Xi'an ya Akademia ya Sayansi ya China Bw. Cao Huitao amesema,

    "Hadi sasa watu bilioni 3.9 duniani hawawezi kupata huduma za mtandao wa Internet. Kwa kuwa mashirika ya upashanaji habari yanapojenga vituo vya huduma hizo, yanazingatia faida zitakazopatikana. Hivyo hayajengi vituo hivyo katika sehemu zisizo na watu wengi kama vile sehemu za ufugaji na jangwa. Hivi sasa mashirika mengi ya nchi mbalimbali yameanza kujenga mfumo wa satilaiti ili kufikisha huduma za mtandao wa Internet mahali popote duniani."

    Shirika la Jiutianweixing liko chini ya taasisi ya utafiti wa mitambo ya mwanga ya hali ya juu ya Xi'an ya Akademia ya Sayansi ya China, na lina teknolojia muhimu za kubuni satilaiti ndogo. Tarehe 2 Februari mwaka huu, satilaiti ya "Vijana NO. 1" iliyobuniwa na shirika hilo ilifanikiwa kurushwa nchini China. Hivi sasa shirika hilo limezindua rasmi mpango wa kurusha satilaiti saba za "Mfumo wa Ladybug" katika nusu ya pili ya mwaka huu. Bw. Cao Huitao anasema,

    "Mpango wetu mpya mwaka huu ni kurusha satilaiti saba kwa roketi moja. Hadi sasa satilaiti tano zimeuzwa, hivyo tumepata fedha za kutosha."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako