• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Zimbabwe kutimiza ahadi kwa marehemu Morgan Tsvangirai

    (GMT+08:00) 2018-02-19 19:01:52

    Rais wa Zimbabwe Emerson Mnangagwa amesema serikali itatimiza ahadi zote za msaada wa kifedha na mali, iliyoitoa kwa waziri mkuu wa zamani ambaye pia alikuwa kiongozi wa chama cha upinzani cha MDC bwana Morgan Tsvangirai.

    Kwa mujibu wa taarifa iliyoandikwa katika gazeti la serikali la New Ziana, akiongea mbele za waombolezaji wakati alipohudhuria msiba huo mjini Harare, bwana Mnangagwa atahakikisha ahadi zote alizozitoa kwa Tsvangirai mwezi uliopita zinatekelezwa, ikiwemo malipo ya gharama zote za matibabu hadi alipofariki.

    Katika hatua nyingine Rais Mnangagwa amesema pindi shughuli za msiba zitakapokamilika, ataijulisha familia ya Tsvangirai ahadi zingine alizotoa wakati alipokutana naye mwezi Januari kwa ajili ya kumjulia hali.

    Rais huyo pia amesema serikali yake itaongoza shughuli zote za msiba huo, na mwili wake utazikwa mjini Buhera siku ya jumanne.

    Akiwa na umri wa miaka 65, Tsvangirai alifariki jumatano iliyopita katika hospital moja mjini Johannesburg nchini Afrika Kusini alikokuwa anatibiwa maradhi ya saratani

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako