• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Viongozi wa EAC watakiwa kuwa kidete swala la mitumba

    (GMT+08:00) 2018-02-20 18:14:28

    Viongozi wan chi za Afrika mashariki wametakiwa kutobadili msimamo wao kuhusu uamuzi wa kupiga marufuku uagiziaji wa nguo kuu kuu.

    Msimamo huo wa kutolegeza kamba katika kudhibiti mitumba, umetolewa na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Baraza la Biashara Afrika Mashariki (EABC), Lilian Awinja alipokuwa anazungumzia yaliyojadiliwa katika mkutano wa bodi ya baraza hilo uliofanyika hivi karibuni jijini Kigali, Rwanda.

    Wakuu wa nchi za EAC ambazo ni Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi na Sudan Kusini, Machi mwaka 2016 walipitisha azimio la nchi wanachama kuachana rasmi na uagizaji wa nguo za mitumba ifikapo mwaka kesho, lengo likiwa ni kulinda viwanda vya ndani.

    Ukiwa umebaki mwaka mmoja kabla ya kuanza kwa azimio la kutoingiza mitumba katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, Marekani kupitia kwa Kaimu Mkuu wa Idara ya Uchumi na Ushirikiano wa Kikanda barani Afrika, Harry Sullivan imedai kuwa, Rwanda, Tanzania na Uganda zinapaswa kufikiria upya uamuzi wake, vinginevyo zinaweza kukabiliana na adhabu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako