• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yajenga reli ya mwendokasi inayounganisha miji ya Beijing na Zhangjiakou

    (GMT+08:00) 2018-02-20 18:56:53

    Mwaka 1905, China ilizindua rasmi ujenzi wa reli inayounganisha miji ya Beijing na Zhangjiakou mkoani Hebei, ambayo ilikuwa reli ya kwanza nchini China iliyojengwa na wachina wenyewe. Zaidi ya miaka mia moja baadaye, reli mpya ya mwendokasi inayounganisha miji hiyo miwili inajengwa, ambayo si kwamba tu itatoa huduma za usafiri kwa ajili ya michezo ya Olimpiki ya mwaka 2022 ya majira ya baridi, bali pia itafungua ukurasa mpya wa reli za mwendokasi nchini China.

    Wafanyakazi wa ujenzi wa reli hiyo wanaendelea na kazi hiyo hata katika wakati huu wa sikukuu ya mwaka mpya wa jadi wa China. Meneja wa Shirika la Ujenzi wa Reli la China Bw. Cheng Duojin anasema,

    "Asilimia 43 ya kazi zimemalizika. Tunatarajia kumaliza kazi zote siku 15 mapema kuliko mpango wa awali."

    Tawi la Chongli la reli hiyo ni kwa ajili ya Michezo ya Olimpiki ya majira ya Baridi ya Beijing ya mwaka 2022. Kwa mujibu wa mpango, ujenzi wa tawi hilo lenye urefu wa kilomita 52 utamalizika mwaka 2019, ili wakati michezo ya Olimpiki itakapofanyika, wachezaji kutoka nchi mbalimbali waweze kufika kwenye makazi yao yaliyoko Chongli moja kwa moja kutoka Beijing kupitia reli hiyo.

    Reli ya mwendokasi inayounganisha miji ya Beijing na Chongli ni sehemu muhimu ya mtandao wa reli za mwendo kasi nchini China. Baada ye kuzinduliwa kwa reli hiyo yenye urefu wa kilomita 173, muda wa safari kutoka Beijing hadi Zhangjiakou utapungua na kuwa dakika 50 kutoka saa zaidi ya tatu.

    Naibu mkuu wa idara ya ujenzi ya shirika linalojenga reli hiyo Bw. Li Yanbo anasema,

    "Ujenzi wa reli hiyo unaendelea vizuri. Hadi sasa tumeshatumia renminbi yuan zaidi ya bilioni 17, ambayo ni asilimia 40 ya uwekezaji wote. Baadaye tutajenga nyumba na majengo mengine ya kuhudumia reli hiyo. Tutahakikisha reli hiyo inazinduliwa mwishoni mwa mwaka 2019."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako