• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Iraq inawashikilia zaidi ya watu 1,500 ambao ni wanawake na watoto kutoka familia za wapiganaji wa IS

    (GMT+08:00) 2018-02-22 18:52:21

    Zaidi ya watu 1,500 wakiwa ni wanawake na watoto kutoka familia za wapiganaji wa kundi la Islamic State wanashikiliwa na mamlaka za nchini Iraq, na serikali ya Iraq inajadiliana na nchi wanazotoka ili kuamua hatma yao.

    Waziri wa masuala ya Jamii wa Iraq Bw. Mohammad al-Sudani amekaririwa na gazeti la al-Mashriq akisema serikali yake inawashikilia wanawake 500 ambao ni wake za wapiganaji wa IS na ikijumlishwa na watoto wanafikia zaidi ya 1500.

    Kwa kuwa imethibitishwa kwamba, mtu yeyote kutoka nje ya Iraq akitenda uhalifu dhidi ya raia wa Iraq, iwe ni kwa kushiriki moja kwa moja ama kwa kusaidia vitendo vya wapiganaji wa IS, basi atahukumiwa kwa mujibu wa sheria ya Iraq, hivyo wanawake ambao watathibitika kuhusika na uhalifu watakabiliwa na mkono wa sheria hiyo.

    Lakini mpaka sasa, serikali ya Iraq imefanya mawasiliano na nchi wanazotoka ili kubaini endapo wanawake hao wanahusika katika uhalifu wa IS, na kuamua hatma ya watoto ambao wanahesabika kutokuwa na hatia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako