• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • BMT yasitisha mamilioni Marathoni RT

    (GMT+08:00) 2018-02-23 08:22:11
    Baraza la michezo la Taifa nchini Tanzania (BMT) limesitisha tozo zote ya mbio za marathoni zilizokuwa zikikusanywa na Shirikisho la Riadha Tanzania (RT).

    Mwaka jana shirikisho hilo lilipitisha tozo mpya ya mbio za marathoni katika kikao kilichoshirikisha waandaaji wake.

    Akizungumza jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa BMT, Mohammed Kiganja amesema wamepata malalamiko ya waandaaji kuhusu malipo wanayotozwa katika mbio za marathoni. Na kuwa wanatarajia kukutana baina ya shirikisho hilo na waandaaji wa mbio zote za marathoni Machi 4 kupitia upya ada hizo. Awali, RT ilipitisha ada elekezi ya kuandaa mbio nchini kulingana na madaraja.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako