• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Nchi za Afrika Mashariki zaadhimisha Siku ya Nile

    (GMT+08:00) 2018-02-23 10:49:13

    Nchi za Afrika Mashariki zimesherehekea Siku ya Nile katika mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa hapo jana na kutoa wito wa hatua endelevu za maendeleo ya Mto Nile.

    Katika kuadhimisha siku hiyo iliyopewa kaulimbiu ya "Nile: Mto wa Pamoja, Hatua za Pamoja", nchi wanachama wa Pendekezo la Bonde la Mto Nile (NBI) zimeeleza nia zao katika kutumia kikamilifu na kwa uendelevu rasilimali za mto huo mrefu zaidi duniani. Mkurugenzi mkuu wa sekretariet ya NBI Innocent Ntabana ametoa wito kwa hatua za pamoja ili kuimarisha uratibu kati ya nchi wanachama na matumizi endelevu ya bonde la mto huo.

    Siku hiyo ni kumbukumbu ya kuanzishwa kwa Pendekezo la Bonde la Mto Nile ambalo linakutanisha nchi 10 zilizoko kwenye bonde la mto huo zikiwemo Ethiopia, Kenya, Tanzania, Sudan Misri, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako