• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Uchaguzi wa wabunge nchini Djibouti wafanyika

  (GMT+08:00) 2018-02-23 19:21:47

  Ijumaa hii Djibouti imefanya uchaguzi wa wabunge ambapo wasimamizi wakisema zoezi hilo limefanyika kwa njia ya amani.

  Waziri mkuu wa nchi hiyo Abdoulkader Mohamed amesema wanasiasa wameendesha kampeni zao kwa njia ya amani bila kutumia lugha za matusi ambazo zingesababisha vurugu.

  Waziri mkuu huyo pia amesema hatua zote katika mchakato huo zimefanyika kwa uwazi na utulivu.

  Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na AU siku ya alhamisi, Waziri mkuu huyo aliikaribisha jumuiya hiyo kupeleka wajumbe wake kushuhudia uchaguzi huo, na kwa kuitikia wito huo AU imepeleka ujumbe wa waangalizi 38 wakiongozwa na waziri mkuu wa zamani wa Jamhuri ya Afrika ya Kati Anicet-Georges Dologuele.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako