Baraza la Serikali la China limesema nchi hiyo itaweka wazi taarifa za shughuli za ustawi wa umma katika miaka mitatu.
Mwongozo uliochapishwa leo na Ofisi Kuu ya Baraza hilo umesema, uwazi zaidi utahakikisha kuwa mgao wa rasilimali katika ustawi wa jamii ni wa haki na usawa, unafanyika katika mazingira yanayohusisha zaidi wananchi, na unaungwa mkono na jamii na pia wanashirikishwa.
Mwongozo huo umechanganua maeneo saba muhimu ya kuongeza uwazi, ikiwemo kuondoa umasikini, elimu, na misaada ya dharura. Katika kuondoa umasikini, mwongozo huo umetaka sera zilizotolewa na mipango pamoja na majina ya miradi, vyanzo vya ufadhili, muda wa mwisho, malengo, matokeo, na watu waliowajibika kutekeleza miradi hiyo viwekwe wazi.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |