• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Baraza la usalama la UN lalaani mashambulizi ya kigaidi Somalia

    (GMT+08:00) 2018-02-27 10:15:56

    Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limelaani vikali mashambulizi mawili ya kigaidi yaliyotokea wiki iliyopita mjini Mogadishu, na kusababisha vifo vya watu 38 na wengine wengi kujeruhiwa.

    Taarifa iliyotolewa na baraza hilo imesema wajumbe wa baraza hilo wametoa salamu za rambirambi kwa familia za wafiwa, wananchi na serikali ya Somalia, na kusisitiza kuwa ugaidi wa aina zote ni moja ya matishio makubwa dhidi ya amani na usalama wa dunia.

    Taarifa pia imesema nchi zote wajumbe wa baraza hilo zimesisitiza kuwa ni lazima kuwafikisha mbele ya sheria wahalifu, waandaaji, watoa fedha na wafadhili wa vitendo vya ugaidi, na nchi zote zinatakiwa kushirikiana na serikali ya Somalia katika kupambana na ugaidi, kwa kufuata sheria za kimataifa, na maazimio ya baraza la usalama la Umoja wa Mataifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako