• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Wizara ya ulinzi wa mazingira ya China yatunga mpango wa kukabiliana na uchafuzi wa hewa

  (GMT+08:00) 2018-02-27 17:48:28

  Wizara ya ulinzi wa mazingira ya China imetoa taarifa ikisema, kupitia usimamizi wa miaka mitano, China imepata maendeleo makubwa katika udhibiti wa uchafuzi wa hewa, huku malengo mbalimbali yaliyowekwa na Mpango wa Operesheni za Kudhibiti na Kukinga Uchafuzi wa Hewa, yakiendelea kutekelezwa. Katika hatua ijayo, wizara hiyo itatunga mpango wa kukabiliana na uchafuzi wa hewa, ili kuhakikisha mafanikio makubwa zaidi yanapatikana katika usimamizi wa uchafuzi wa hewa.

  Wizara ya ulinzi wa mazingira ya China imetoa taarifa ikisema, katika muda wa miaka mitano iliyopita China imeondoa uzalishaji wenye uwezo mdogo katika kuhifadhi mazingira, kuharakisha usafishaji wa nishati, kudhibiti idadi ya jumla ya matumizi ya makaa ya mawe, kuhimiza mageuzi kwenye shughuli za saruji, mafuta na vitu vya kikemikali na kuimarisha uwezo wa kusimamia mazingira ya hewa. Sifa ya jumla ya hewa ya China imeboreshwa kupitia hatua hizo. Mkurugenzi wa idara ya usimamizi wa mazingira ya hewa ya wizara hiyo Bw. Liu Bingjiang anasema,

  "Mwaka jana, kiwango cha PM 2.5 cha eneo la mji ya Beijing, Tianjin na mkoa wa Hebei, eneo la delta ya mto wa Yangtze na eneo la mto wa Zhu kimepungua kwa asilimia 39.6. 34.3 na 27.7 mtawalia ikilinganishwa na cha mwaka 2013. Kiwango cha PM2.5 cha eneo la mto Zhu kimefikia kigezo kwa miaka mitatu mfululizo wa. Malengo yote ya kuboresha hewa yaliyowekwa yametimizwa."

  Bw. Liu amesema, ingawa kazi ya kudhibiti na kukinga uchafuzi wa hewa imepata maendeleo katika kipindi hicho, lakini tatizo la uchafuzi wa hewa bado ni kubwa katika baadhi ya sehemu na baadhi ya wakati. Katika hatua ijayo, wizara hiyo itatunga mpango wa miaka mitatu wa kushinda mapambano dhidi ya uchafuzi huo. Bw. Liu anasema,

  "Hatua halisi ni pamoja na kuzuia na kudhibiti kutakakotilia maanani kutatua suala la utaratibu wa viwanda, utaratibu wa nishati na utaratibu wa mawasiliano. Katika upande wa utaratibu wa viwanda, serikali itaendelea kushughulikia kampuni zinazoleta uchafuzi, kugeuza uwezo wa ziada wa uzalishaji na kuhamisha viwanda vinavyotoa uchafuzi mkali kutoka mijini, huku ikiimarisha usimamizi wa utekelezaji wa sheria ya ulinzi wa mazingira. Kwenye upande wa kurekebisha utaratibu wa nishati, serikali itashughulikia makaa ya mawe na kuendelea kudhibiti ujumla wa matumizi ya makaa. Kwa upande mwingine wa utaratibu wa mawasiliano, serikali itazingatia kurekebisha usafirishaji kwa njia ya barabara kuu na reli, na kuinua vigezo vya kudhibiti utoaji wa moshi wa magari na meli."

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako