• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serikali ya Tanzania yasema vikwazo vya kibiashatra vilivyokuwapo kati ya Tanzania na Kenya vimeshaondolewa

    (GMT+08:00) 2018-02-27 19:05:04

    Serikali ya Tanzania imesema vikwazo vya kibiashara vilivyokuwapo kati yake na Kenya vimeshaondolewa,isipokuwa kimebaki cha uingizaji mahindi katika mji wa Mombasa nchini Kenya.

    Hatua hiyo imetokana na maelekezo ya rais John Pombe Magufuli aliyoyatoa wiki iliyopita kwenye mkutano wa wakuu wa jumuiya ya Afrika Mashariki.

    Rais Magufuli aliwataka mawaziri wa nchi hizo kumaliza tofauti za kibiashara zilizopo.

    Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirkiano wa Afrika Mashariki ,Prof Adolf Mkenda aliyasema hayo wakati mkutano uliowakutanisha wafanyabiashara na Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF) ,uliohusu wiki ya Tanzania nchini Kenya ulioandaliwa na Balozi wa Tanzania nchini Kenya Pindi Chana.

    Kuhusu wiki ya Tanzania nchini Kenya,Prof Mkenda alisema itaadhimishwa Aprili 26 mwaka huu na itahusisha maonyesho ya bidhaa zinazozalishwa Tanzania.

    Alisema hivi sasa Tanzania ina mkakati wa kushika soko la Kenya pamoja na kutangaza bidhaa zake kwa kuzipeleka kwa wingi kama vile vitenge,korosho,na dawa za kusafishia meno.

    Kwa upande wake Balozi Chana alisema wafanyabiashara wa viwandani na mkononi wanakaribishwa katika tamasha hilo,lengo kuu likiwa ni kutangaza bidhaa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako