• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sekta ya uzalishaji nchini China inaongezeka kwa taratibu

    (GMT+08:00) 2018-02-28 18:42:03

    Sekta ya uzalishaji nchini China imeendelea kupanuka kwa kasi ndogo mwezi Februari huku viwanda vya teknolojia ya juu vikikua kwa nguvu.

    Mamlaka ya Takwimu ya China imesema, alama ya kusimamia manunuzi ya sekta ya uzalishaji ilifikia 50.3 mwezi huu, ikiwa ni chini kutoka 51.3 ya mwezi Januari.

    Mtakwimu wa ngazi ya juu wa Mamlaka hiyo Zhao Qinghe ameelezea kushuka huko kuwa ni kwa kawaida kwa kuwa alama hiyo ina kawaida ya kushuka katika mwezi wa sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa Kichina.

    Bw. Zhao amesema alama hiyo kwenye viwanda vya teknolojia ya juu imefikia 54 mwezi huu, ikilinganishwa na 53.2 kwa mwezi Januari, ikiwa ni ya juu zaidi ya 50.3 ya sekta nzima ya uzalishaji.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako