Mjumbe wa kudumu wa China katika Ofisi ya Umoja wa Mataifa mjini Geneva Bw. Yu Jianhua ametoa wito wa juhudi za pamoja kufanywa kuhimiza ujenzi wa jumuiya yenye hatma ya pamoja, na kuanzisha utaratibu wa kusimamia haki za binadamu duniani wenye haki, usawa, uwazi na ushirikishi.
Akihutubia Mkutano wa 37 wa Baraza la haki za kibinadamu katika Umoja wa Mataifa, Bw. Yu Jianhua ametoa mapendekeo ya kuhimiza haki za binadamu kwa njia ya kuchochea maendeleo, kuleta usalama, kukuza ushirikiano na kulinda haki na usawa.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |