Idara kuu ya usimamizi wa viwanda na biashara ya China imetoa taarifa ikisema, hivi karibuni hatua za mageuzi ya mfumo wa kibiashara zilizochukuliwa na serikali ya China zimepunguza kigezo cha kuingia katika soko na kuhamasisha uhai wa soko. Mwaka jana, idadi ya kampuni mpya zinazoandikishwa kwa siku nchini China imefikia elfu 16.6, huku nafasi ya mazingira ya kibiashara ya China duniani imeinuliwa kwa alama 18.Mkurugenzi wa idara kuu ya usimamizi wa viwanda na biashara ya China Bw. Zhang Mao, amesema mageuzi ya mfumo wa kibiashara wa China yamepata mafanikio na wadau wa soko wamedumisha mwelekeo wa maendeleo ya kasi. Anasema,
"Idadi ya wadau wa soko la China iliongezeka kwa elfu 31 kila siku mwaka 2013, na sasa idadi hiyo imefikia elfu 52. Idadi ya kampuni mpya zilizoandikishwa kwa siku imeongezeka kutoka 6900 ya mwaka 2013, hadi kufikia elfu 16.6 ya hivi sasa. Idadi ya kampuni kwa watu elfu moja nchini China pia imeongezeka maradufu kutoka 10 hadi 21. Kwa kufuatia tathmini ya Benki ya Dunia, katika upande wa urahisi wa kluandikisha kampuni, nafasi ya soko la China imeongezeka kwa alama 65 kati ya masoko 180 duniani."
Hadi sasa idadi ya wadau wa soko la China imefikia milioni 99.6, ambayo inatarajiwa kuzidi milioni mia moja mwezi wa Machi. Bw. Zhang amesema, katika hatua ijayo serikali ya nchi hiyo itaendelea kulegeza vigezovya kuingia katika soko, na kuinua kiwango cha urahisi wa uandikishaji wa kampuni.
"Ya kwanza ni kuhimiza kwa pande zote sera ya kutenganisha kibali na leseni. Katika nusu ya kwanza ya mwaka huu, tutafanya jaribio kwenye eneo la maendeleo la sehemu mbalimbali, eneo la viwanda vya teknolojia ya juu, eneo jipya la ngazi ya taifa na maeneo mengi yenye sharti linalofaa, hivi sasa miji na sehemu zaidi ya mia moja zimefanyiwa jaribio. Kwa mujibu wa mpango, katika nusu ya pili ya mwaka huu, tutazidi kupunguza utaratibu baada ya kupata leseni, ili kuzifanya kampuni kuingia katika hali ya uendeshaji haraka iwezekanavyo. Halafu tutafanya juhudi kuhimiza mchakato wa uandikishaji wa kielektroniki na leseni ya uendeshaji ya kielektroniki. Hatimaye tutazidi kurahisisha mfumo wa kujitoa kutoka kwenye soko."
Mbali na hayo, Bw. Zhang ameongeza kuwa, idara hiyo pia itaendelea kuboresha mfumo wa usimamizi wa soko, kuimarisha mawasiliano ya habari na adhabu dhidi ya udanganyifu, kuzidisha usimamizi wa uaminifu wa kampuni, na kuboresha njia ya kutoa malalamiko ya wateja.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |