• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ajenda kuu ya "Mikutano Miwili" ya China mwaka 2018

    (GMT+08:00) 2018-03-02 10:12:43

    Mikutano miwili ya mwaka, ambayo ni Mkutano wa bunge la umma la China na Mkutano wa baraza la mashauriano ya kisiasa, itakayoanza wiki ijayo ina umuhimu mkubwa mwaka huu, baada ya China kutangaza rasmi imeingia katika zama mpya.

    Mkutano wa kwanza wa awamu ya 13 ya Bunge la Umma la China NPC, na Mkutano wa kwanza wa awamu ya 13 ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China CPPCC, inayojulikana kwa pamoja kuwa ni "Mikutano Miwili" itafunguliwa tarehe 3 na tarehe 5 mwezi huu mjini Beijing.

    Mwaka huu kwa mara ya kwanza Mikutano Miwili itafanyika kwa kuelekezwa na mtazamo wa ujamaa wenye umaalumu wa Kichina katika zama mpya uliotolewa na rais Xi Jinping wa China, ambayo itakuwa na mambo kadhaa yatakayowavutia wananchi.

    Mambo hayo ni pamoja na wazo jipya la rais Xi Jinping kuhusu ujamaa wenye umaalumu wa China katika zama mpya lililotolewa katika Mkutano wa awamu ya 19 ya kamati kuu ya chama cha kikomunisti cha China CPC, viongozi wa serikali ya awamu mpya, njia mpya za kupambana na ufisadi, malengo mapya ya ongezeko la uchumi na kupunguza umaskini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako