• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Viongozi wa vyama na wataalamu wa nchi za Afrika Mashariki watoa pongezi kwa mfumo wa kisiasa na maendeleo ya uchumi wa China

  (GMT+08:00) 2018-03-02 10:41:32

  Wataalamu wa majopo ya washauri bingwa ya Kenya, Tanzania na Uganda walipohojiwa na mwandishi wetu wa habari kabla ya kufunguliwa kwa mikutano ya mwaka 2018 ya Bunge la Umma la China na Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China, wametoa pongezi kwa mfumo wa mikutano hiyo miwili, maendeleo ya uhusiano kati ya China na Afrika na mambo mbalimbali.

  Katibu mkuu wa chama tawala cha Jubilee cha Kenya Bw. Raphael Tuju amesema Kenya haiwezi kufuata moja kwa moja utaratibu wa kisiasa na kidemokrasia ya nchi za magharibi, itajifunza uzoefu wa China katika ujenzi wa taifa na vyama, na kutafuta njia ya kujiendeleza inayoendana na hali ya Kenya, akisema,

  "China ina watu bilioni 1.3 lakini wameweza kuwa na mfumo ambao umefanya nchi hiyo kuwa tulivu. Na ndio maana naona sisi wakenya tuna mengi ya kujifunza kutoka kwao. Nchi yetu pia ina changamoto tofauti, tuna makabila tofauti na dini kama vile tu China, lakini wameweza kuwa na mpango ambao unawafaa. Ambao unazingatia tamaduni na maisha ya kila siku ya watu wa China. Hivyo nadhani mojawapo wa mambo ambayo yanatuvutia kwenye mfumo wa China na utawala ni kwamba unawafaa. Kwa hivyo naona inawafaa sana na kweli ina umaalum wa kichina".

  Mtaalamu wa siasa wa Chuo Kikuu cha Kenyatta Prof. Otiato Wafula amesema ujamaa wenye umaalum wa kichina umeingia kipindi kipya, na unalenga kutimiza maisha bora ya wananchi na ustawi wa taifa. Ingawa hali za China na nchi za Afrika zinatofautiana, lakini nchi zote zinabeba majukumu ya kuendeleza uchumi, kuboresha maisha ya watu, na kuondoa umaskini. Mawazo ya ujamaa wenye umaalum wa kichina katika zama mpya na mfumo wa bunge la umma la China ni uhakikisho wa kisiasa wa maendeleo ya kasi ya China, akisema,

  "Hapo ambapo wamefika wamejiweza kiuchumi, wamejiweza kimasomo, kiteknolojia, sasa wamepita huu mpaka, haswa ukiangalia katika miaka arobaini Mchina tayari alishajikomboa kifikra, mchina wa kawaida anajua wamesimama wapi kama watu wa China, umeingilia akili za watu kwa huu ujamaa wake, wamefaulu kwa kiwango kikubwa sana. Lakini ukiangalia utamaduni na itikadi za mwafrika ni itikadi za kijamii, mimi ni mtu ambaye nakubali ya kwamba mchina atabaki kuwa mchina na atatetea uchina wake."

  Alipozungumzia athari ya uchumi wa China na fedha za China Renminbi kwa Afrika, mtaalamu wa kituo cha uhusiano wa kidiplomasia cha Tanzania Prof. Innocent Shoo amesema ongezeko la biashara kati ya China na Afrika limeleta mahitaji ya matumizi ya fedha za China, na fedha hizi zimekubaliwa zaidi na nchi za Afrika, akisema,

  "China ndiyo nchi ya pili kwa ukubwa wa GDP duniani, China pesa yake currency inaitwa Yuan sasa hivi imeingia kama pesa ya kimataifa duniani kwamba unaweza ukafanya biashara popote kwa kutumia Yuan, sasa kuna mkakati mkubwa sana kwa taifa la China kuongea na serikali za Afrika kuhakikisha kwamba kwenye benki zetu kuu zinakuwa zinaweka akiba ya Yuan ya pesa za China. Kwa hiyo hii itasaidia wafanyabiashara wengi sana wa Afrika ambao watakuwa wanaenda China wanachukua hela za China kutoka nazo Afrika wanaenda nazo moja kwa moja China wananunua bidhaa na kurudi nazo."

  Mhariri wa habari za kisiasa kutoka Uganda Bw. Andrew Mwenda amesema ingawa hali ya duniani inabadilikabadilika, China ikiwa nchi yenye watu zaidi ya bilioni 1.3, uchumi wake umekuwa unapata maendeleo kwa utulivu. Ushirikiano kati ya China na Afrika unaolenga kunufaishana utaisaidia Afrika kujiendeleza katika sekta za viwanda na kilimo, na kutimiza maendeleo endelevu ya uchumi kwa kujitegemea, akisema,

  "Tangu China ianze sera ya mageuzi na ufuguaji mlango mwaka 1978, soko la mitaji limefungua hatua kwa hatua, uchumi wa kiserikali na binafsi umepata maendeleo kwa pamoja, na ujenzi wa uchumi umepata mafanikio ya kihistoria, mambo hayo yameonesha kuwa Chama cha Kikomunisti cha China kimetawala vizuri sana. Nchi nyingi za Afrika zitanufaika kutoka uchumi wa China unaostawi na ushirikiano kati ya China na Afrika unaoimarika siku hadi siku."

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako