• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yaitaka Marekani kubadilisha njia ya kushughulikia suala la Korea

    (GMT+08:00) 2018-03-02 14:17:27

    Mwanadiplomasia mwandamizi wa China ameitaka Marekani kubadilisha njia inayotumia kushughulikia suala la Korea na kusema "suala la nyuklia la peninsula ya Korea limepamba moto na kufikia hatua ya kuwa hatari kwa usalama wa dunia.

    Bi. Fu Ying ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya mambo ya nje ya bunge la umma la China, amesema kwenye makala iliyochapishwa kwenye gazeti la Daily Telegraph la Uingereza kuwa, Marekani na washirika wake wanaangalia zaidi vikwazo vinavyoweza kuwekwa dhidi ya Korea Kaskazini kuliko hali ya usalama ya nchi hiyo baada ya kuacha mpango wake wa nyuklia. Amesema vikwazo vimeathiri sana uchumi wa Korea Kaskazini, lakini vimeshindwa kuzuia mpango wake wa nyuklia na makombora.

    Habari pia zinasema Rais Moon Jae-in wa Korea Kusini amefanya mazungumzo na Rais Donald Trump wa Marekani na kukubaliana kuendelea na juhudi za kuifanya Peninsula ya Korea kuwa eneo lisilo na silaha za nyuklia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako