• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa kwanza wa Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la awamu ya 13 la China kufanyika Machi 3 hadi 15

    (GMT+08:00) 2018-03-02 17:45:25

    Msemaji wa mkutano wa kwanza wa Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la awamu ya 13 la China Bw. Wang Guoqing amesema, mkutano huo utafunguliwa saa tisa alasiri kesho na utafungwa tarehe 15 asubuhi.

    Mwaka huu ajenda kuu ya mkutano huo ni pamoja na kusikiliza na kujadili ripoti ya kazi ya kamati ya kudumu ya baraza la mashauriano ya kisiasa la China na ripoti kuhusu hali ya mapendekezo; kuhudhuria mkutano wa kwanza wa Bunge la Umma la Awamu la 13 la China na kusikiliza na kujadili mswada wa marekebisho ya katiba na mswada wa sheria ya usimamizi. Pia kujadili na kupitisha katiba ya mkutano wa Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China, mapendekezo na ripoti za mkutano huo; kuchagua mwenyekiti, naibu mwenyekiti, katibu mkuu na wajumbe wa kudumu wa kamati ya baraza hilo.

    Bw. Wang pia amesema, maandalizi yote ya mkutano huo yamekamilika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako