• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa kwanza wa awamu ya 13 ya Bunge la Umma la China kufunguliwa kesho

    (GMT+08:00) 2018-03-04 12:53:41

    Mkutano wa kwanza wa Bunge la 13 la Umma la China NPC utafanyika kuanzia kesho tarehe 5 hadi tarehe 20 hapa Beijing. Huo utakuwa ni mkutano utakaofanyika kwa muda mrefu zaidi na kujadili ajenda nyingi zaidi katika miaka ya karibuni.
    Kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo asubuhi, msemaji wa mkutano huo Bw. Zhang Yesui amefahamisha kuwa, mkutano huo wa NPC utakuwa na ajenda 10, ambazo ni kuthibitisha Ripoti ya kazi ya serikali, kuthibitisha Ripoti kuhusu mipango na Ripoti ya bajeti, kuthibitisha Muswada wa marekebisho ya katiba, kuthibitisha Muswada wa sheria ya uendeshaji wa mashitaka, kuthibitisha Ripoti ya kazi ya Halmashauri ya kudumu ya Bunge la umma, Ripoti ya kazi ya Mahakama kuu ya umma, Ripoti ya kazi ya Idara kuu ya uendeshaji wa mashitaka ya umma, kuthibitisha Muswada wa mageuzi ya vyombo vya Baraza la serikali, na kuchagua na kuamua uteuzi wa viongozi wa vyombo vya serikali.
    Habari zinasema mkutano huo wa NPC utaitisha mikutano 14 na waandishi wa habari kuhusu marekebisho ya katiba, utungaji wa sheria wa Bunge la Umma, kazi za usimamizi na matatizo yaliyopo katika ukuaji wa uchumi na jamii. Na baada ya kufungwa kwa mkutano huo asubuhi wa tarehe 20, waziri mkuu wa awamu mpya atakutana na waandishi wa habari wa China na nchi mbalimbali.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako