• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa Bunge la Umma la China kufunguliwa kesho

    (GMT+08:00) 2018-03-04 12:59:08
    Mkutano wa kwanza wa awamu ya 13 ya Bunge la Umma la China NPC utafunguliwa tarehe 5 na kufungwa tarehe 20. Huo utakuwa ni mkutano wa bunge utakaofanyika kwa muda mrefu zaidi na kujadili ajenda nyingi zaidi katika miaka ya karibuni.

    Kwenye mkutano na waandishi wa habari wa mkutano huo ulifanyika leo asubuhi, msemaji wa mkutano huo Bw. Zhang Yesui amefahamisha kuwa, mkutano huo wa NPC utajadili ajenda 10, utasikiliza na kujadili ripoti ya kazi ya serikali, kukagua na kupitisha ripoti kuhusu mipango, pamoja na ripoti ya bajeti, kujadili mswada wa marekebisho ya katiba, kuchagua na kuteua watumishi wa umma wa serikali na nyinginezo.

    Habari zinasema mkutano huo wa NPC utaandaa mikutano 14 na waandishi wa habari kuhusu marekebisho ya katiba, utungaji wa sheria ya Bunge la Umma, kazi za ukaguzi na maswala mengine makuu yanayohusu maendeleo ya uchumi na jamii. Na baada ya kufungwa kwa mkutano huo asubuhi wa tarehe 20, waziri mkuu wa awanu mpya atakutana na waandishi wa habari wa China na nchi za nje.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako