• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa maandalizi ya mkutano wa kwanza wa Bunge la 13 la Umma wafanyika hapa Beijing

    (GMT+08:00) 2018-03-04 19:29:33

    Mkutano wa maandalizi ya mkutano wa kwanza wa Bunge la 13 la Umma leo umefanyika hapa Beijing. Mkutano huo umechagua Jopo la wenyeviti na katibu mkuu, huku ukipitisha ajenda za mkutano wa kwanza wa Bunge la 13 la Umma.

    Mkutano wa Bunge la 13 la Umma la China una wajumbe 2980. Hadi kufikia Machi 3, wajumbe 2976 wameandikishwa katika ofisi ya sekretarieti ya mkutano huo. Wajumbe 2951 wamehudhuria mkutano huo wa maandalizi na wengine 29 hawakuhudhuria, ambapo idadi ya mahudhurio imefikia akidi.

    Mwenyekiti wa Bunge la 12 la Umma la China Bw. Zhang Dejiang ameendesha mkutano huo akitangaza kuwa mkutano wa kwanza wa Bunge la 13 la Umma la China utafanyika kesho tarehe 5, na maandalizi ya mkutano huo yamekamilika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako