Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang amesema katika muda wa miaka mitano iliyopita, wachina milioni 68 wameondokana na umaskini, watu milioni 8.3 wamehama kutoka sehemu zenye hali duni kijiografia, idadi ya watu maskini kati ya watu wote nchini China imepungua kuwa asilimia 3.1 kutoka asilimia 10.2, mapato ya wakazi yanaongezeka kwa asilimia 7.4 kwa mwaka, ongezeko ambalo ni kubwa zaidi kuliko lile la uchumi, na China imekuwa na idadi kubwa zaidi ya watu wenye mapato ya kati duniani. Idadi ya watu wanaotalii nje ya China imeongezeka na kufikia watu milioni 130 kutoka milioni 83. China pia imekuwa na watu wengi zaidi wanaopata dhamana ya jamii, ambapo watu milioni 900 wanashiriki kwenye bima ya matunzo ya uzeeni, na bilioni 1.355 wameshiriki kwenye bima ya matibabu. Wastani wa umri wa kuishi kwa wananchi wa China umefikia miaka 76.7.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |