Ripoti ya kazi ya serikali imekadiria kuwa thamani ya jumla ya uzalishaji mali nchini China itaongezeka kwa 6.5% mwaka huu; kiwango cha CPI kitapanda kwa 3% hivi; idadi ya nafasi mpya za ajira itaongezeka kwa watu milioni 11 na zaidi, na uchunguzi wa watu wenye ukosefu wa ajira mijini kitakuwa ndani ya 5.5%, na kiasi cha watu waliojiandikisha kukosa ajira mijini ni ndani ya 4.5%.
Ripoti hii imedhihirisha kuwa, uchunguzi wa watu wanaokosa ajira mijini unahusisha wakazi wa kudumu wakiwemo wakulima wanaofanya kazi za vibarua mijini, mwaka huu ni mara ya kwanza kuweka kiwango hiki kiwe lengo la makadirio, ili kuonesha kwa pande zote hali ya watu wanaopata ajira, na kuonesha matakwa ya kuwawezesha watu wote wanufaike pamoja na maendeleo ya uchumi.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |