Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang ametoa ripoti ya kazi ya serikali akisema, mwaka huu China itapunguza watu maskini zaidi ya milioni 10 vijijini na kukamilisha kazi ya kuwahamishia watu wanaoishi kwenye mazingira yenye hali ngumu milioni 2.8 katika sehemu nyingine ili kuboresha maisha yao.
Amesema, China inatakiwa kuhimiza kazi ya kuwasaidia watu maskini wajiendeleze kwa kupitia viwanda, elimu, afya na ulinzi wa mazingira ya asili, kuziba pengo kwenye miundombinu na huduma za umma, na kuchochea nguvu zao wenyewe za kuondokana na umaskini.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |