• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yahimiza kwa pande zote kutawala nchi kwa kufuata katiba na kufuata sheria

    (GMT+08:00) 2018-03-05 11:26:26

    Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang amesema, China itahimiza kwa pande zote kufanya utawala wa nchi kwa kufuata katiba na kufanya mambo ya utawala kwa mujibu wa sheria, na itaharakisha kujenga serikali inayofanya mambo ya utawala kwa mujibu wa sheria na kuinua kwa pande zote uwezo na ufanisi wa serikali.

    Bw. Li amesema, China itaweka kwa pande zote shughuli za serikali katika njia ya utekelezaji wa kisheria na kuhimiza uwazi wa mambo ya utawala. Pia itaimarisha usimamizi na ukaguzi wa kazi za uhasibu, ili kuweka madaraka ndani ya kizimba cha utaratibu, na kutoa adhabu kali kwa vitendo mbalimbali vya ufisadi. China itaboresha muundo wa vyombo vya serikali na wajibu na majukumu yao, na kuzidisha mageuzi ya vyombo vya serikali; itaunda mfumo wa usimamizi wa serikali wa kubainisha wajibu na majukumu, na kufanya mambo ya utawala kwa mujibu wa sheria, ili kuimarisha imani ya watu juu ya serikali na kuongeza uwezo wa na utendaji wa serikali.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako