• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yapenda kujiunga na nchi mbalimbali katika kuhimiza ujenzi wa Jumuiya ya Mustakabali wa pamoja wa binadamu

    (GMT+08:00) 2018-03-05 11:30:17

    Ripoti ya waziri mkuu kuhusu kazi ya serikali imedhihirisha kuwa, China itafuata siku zote bila kulegalega njia ya kujiendeleza kwa amani, na kuhimiza ujenzi wa uhusiano wa kimataifa wa aina mpya. China inapenda kujiunga pamoja na nchi mbalimbali katika kuhimiza ujenzi wa Jumuiya ya Mustakabali wa pamoja wa binadamu.

    Ripoti hii imesema, China itafanya juhudi za kushiriki kwenye mageuzi na uboreshaji wa kazi ya kushughulikia mambo ya dunia nzima, na itajikita katika kujenga uchumi wa dunia wa kufungua mlango. China itasukuma mbele uratibu na ushirikiano kati ya nchi kubwa, kuendeleza kwa kina ujirani mwema na urafiki na nchi majirani ili kutafuta maendeleo kwa pamoja, na kuimarisha mshikamano na ushirikiano na nchi zinazoendelea. China itaendelea kufanya kazi yake ya nchi kubwa inayowajibika kwa ajili ya kutatua matatizo ya kimataifa na kikanda. Na itakamilisha mfumo wake wa uhakikisho wa usalama wa maslahi yake katika nchi za nje.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako