Ripoti ya kazi za serikali inayothibitishwa leo kwenye Bunge la umma la China inaonesha kuwa mwaka huu China itapanua uagizaji bidhaa kutoka nje, na kuhimiza biashara huria na urahisi wa uwekezaji.
Ripoti hiyo imedokeza kuwa China itafanya maonesho ya kwanza ya kimataifa ya bidhaa zinazoagizwa kutoka nje, kupunguza ushuru wa magari na baadhi ya bidhaa zinazotumiwa katika maisha ya kila siku, China inapanga kumaliza mazunguzo ya kujenga uhusiano wa wenzi wa kiuchumi wa kikanda katika pande zote mapema iwezavyo, na kuharakisha ujenzi wa eneo la biashara huria la Asia na Pasifiki na Umoja wa uchumi wa Asia Mashariki. Ripoti hiyo pia imesisitiza kuwa China inapendekeza kutatua mikwaruzano ya kibiashara kwa majadiliano yenye usawa, kupinga vitendo vya kujilinda kibiashara, na kushikilia kulinda maslahi yake halali.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |