• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri mkuu wa China atoa ripoti ya utendaji wa serikali katika mkutano wa kwanza wa bunge la 13 la umma la China

    (GMT+08:00) 2018-03-05 17:48:26

    Mkutano wa kwanza wa bunge la 13 la umma la China umefunguliwa leo hapa Beijing. Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang ametoa ripoti ya utendaji wa serikali katika miaka mitano iliyopita, huku akitoa mapendekezo kwa ajili ya utendaji wa serikali kwa mwaka huu.

    Kwenye ripoti ya utendaji wa serikali, Bw. Li Keqiang amefanya majumuisho kuhusu utendaji wa serikali katika miaka mitano iliyopita. Amesema pato la taifa la China GDP ilifikia yuan trilioni 82.7 kutoka yuan trilioni 54, na kushuhudia ongezeko la asilimia 7.1 kwa mwaka. Ongezeko hilo limefanya mchango wa China kwa uchumi wa dunia uwe zaidi ya asilimia 30. Katika kipindi hicho mtandao wa reli ya mwendo kasi, biashara ya mtandao wa Internet, mbinu ya malipo kwenye simu za mkononi, na uchumi wa kuchangia umeongoza kote duniani. Na idadi ya watu maskini nchini China imepungua kwa zaidi ya watu milioni 68. Bw. Li Keqiang amesema:

    "katika miaka mitano iliyopita, tumekutana na matatizo mengi, na hatari na changamoto mbalimbali zilifuatiana, kumetokea mambo mbalimbali ambayo hatujawahi kukumbana nayo tangu tuanze kutekeleza mageuzi na kufungua mlango. Mafanikio ya mageuzi ya China hayakupatikana kwa u urahisi. Hayo ni matokeo ya uongozi wa kamati kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China inayoongozwa na rais Xi Jinping, ni matokeo ya maelekezo ya wazo la rais Xi Jinping la ujamaa wenye umaalumu wa China katika zama mpya, pia ni matokeo ya mshikamano wa watu wote wa China."

    Kwenye ripoti yake Bw. Li Keqiang amesema, mwaka huu inakadiriwa kuwa pato la taifa la China litaongezeka kwa 6.5%, kiwango cha bei ya bidhaa CPI kitapanda kwa 3% hivi; idadi ya nafasi mpya za ajira itaongezeka kwa milioni 11 na zaidi, na watu wenye ukosefu wa ajira mijini kwa mujibu wa uchunguzi kitakuwa ndani ya 5.5%, na kiasi cha watu waliojiandikisha kukosa ajira mijini ni ndani ya 4.5%.

    Ripoti hii imedhihirisha kuwa, uchunguzi wa watu wasio na ajira mijini unahusisha wakazi wa kudumu wakiwemo wakulima wanaofanya kazi za vibarua mijini, mwaka huu ni mara ya kwanza kuweka kiwango hiki kiwe lengo la makadirio, ili kuonesha kwa pande zote hali ya watu wanaopata ajira, na kuonesha matakwa ya kuwawezesha watu wote wanufaike na maendeleo ya uchumi.

    Mwaka huu China inaadhimisha miaka 40 tangu ianze kutekeleza sera ya mageuzi na kufungua mlango, ni mwaka wa kwanza wa utekelezaji wa matokeo ya mkutano mkuu wa 19 wa chama cha kikomunisti cha China, pia ni mwaka muhimu wa kujenga China kuwa jamii yenye maisha bora. Ripoti hii imesisitiza kuwa,

    "kwanza ni kuhimiza maendeleo yenye sifa bora. Ni lazima kutilia maanani kutatua suala la kutokuwa na uwiano katika maendeleo, kujenga mfumo wa uchumi wa kisasa, kuhimiza kuboresha miundo ya uchumi, na kuhakikisha ongezeko la uchumi liwe mwafaka. Pili, kuongeza nguvu ya mageuzi na kufungua mlango. Tatu, kutatua masuala matatu makuu ya kujenga jamii yenye maisha bora. Kuhakikisha kazi ya kuondoa umaskini inaekelezwa kwa pande zote, kuhakikisha sifa ya mazingira inaboreshwa. Kushikilia wazo la kujiendeleza kwa kuzingatia watu, kutatua mambo yote yanayofuatiliwa na kusumbua watu, kuhimiza haki na usawa wa jamii na maendeleo ya pande zote ya binadamu, ili maisha ya watu yaboreshwe zaidi kutokana na maendeleo ya nchi. "

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako