Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang jana alitoa ripoti ya kazi ya serikali kwenye Mkutano wa kwanza wa awamu ya 13 ya Bunge la Umma la China, akijumuisha kazi zilizofanywa na serikali katika miaka mitano iliyopita, na kuweka mipango kwa kazi ya serikali ya mwaka 2018.
Shirika la habari la Uingereza Reuters linaona kudumisha ongezeko endelevu la uchumi kutakuwa ni kazi kuu kwa China kutimiza malengo yake.
Shirika la habari la Marekani AP limeripoti hatua za China za kuhimiza mageuzi wa kimuundo kwenye upande wa ugavi, na kuharakisha mchakato wa kuijenga China kuwa nchi yenye nguvu ya uzalishaji.
Shirika la habari la Russia RT linafuatilia zaidi sera ya ufunguaji mlango ya China, hususan hatua za China kuhimiza kwa hatua madhubuti ongezeko la uwekezaji wa nje.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |